Thursday, November 10, 2016

Wadau na wanasoka mbalimbali walivyoupokea ushindi wa Trump

1

Donald Trump amechaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani akimbwaga Hillary Clinton kuingia Ikulu ya White House.

Ushndi huo umepokelewa kwa hisia tofauti tofauti na wadau wa soka duniani, angalia Tweets za wadau mbalimbali wa soka baada ya ushindi wa Trump.

Azam wamuenzi vyema Mzee Said Mohamed, yatoa kipigo kitakatifu kwa Mwadui


AZAM FC leo wamemuenzi vyema Mzee Said Mohamed kwa kuishushia kipigo cha mbwa mwizi Mwadui FC cha mabao 4-1, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga.
Katika mchezo huo ambao timu zote mbili zilianza kwa hofu kubwa kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo yao iliyopita, Mwadui walipata goli dakika ya 20 kupitia kwa Jerryson Tegete lakini mwamuzi alikataa kwa madai kwamba aliunawa kabla ya kufunga.
Haikuishia hapo, Hassan Kabunda akaweka goli safi kwa bicycle kick dakika ya 30 na kuwapa Azam FC wakati mgumu.
Dakika ya 36 Azam FC walifanya mabadiliko baada ya Mudathir Yahya kutoka kufuatia kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Singano.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Mwadui kutoka kifua mbele katika uwanja wao wa nyumbani.
Azam walifanya tena mabadiliko kwa kumtoa Gadiel Michael na nafasi yake kuchukuliwa na Shaaban Idd mnamo dakika ya 53 na baadaye mabadiliko mengine kufanywa kwa kutoka Frank Domayo na kuingia Francisco Zekumbawira.
Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na mtazamo chanya baada ya Azam FC kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa John Bocco dakika ya 54 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Mwadui.
Shaaban Idd aliyeingia kutoka benchi aliipatia Azam bao la pili dakika ya 71, huku Mzimbabwe Zekumbawira ambaye pia aliingia kutokea benchi akifunga bao la tatu dakika ya 74.
Shaaban Idd kwa mara nyingine tena aliipa Azam bao la nne dakika ya 77 na kuvunja matumaini yote ya Mwadui ya kushinda mchezo huo uliofanyika katika dimba lao la nyumbani.
Matokeo yanaifanya Azam FC kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikijikusanyia pointi 25 ikizidiwa 10 tu na vinara Simba waliojikusanyia 35, ambao jioni ya leo wamepoteza mchezo kwa kufungwa na Tanzania Prisons mabao 2-1, huku Mwadui wakiwa kwenye nafasi ya 14 na alama zao 13.

Lebron James asimamishwa.


Haikutegemewa lakini imetokea. Cleveland Cavs wamefungwa na Atlanta Hawks huku wakiwa na rekodi bora zaidi katika NBA msimu huu.
Dennis Schroder alifunga pointi nyingi zaidi katika maisha yake ya mchezo wa kikapu, 28 points na Atlanta Hawks ikaifunga Cleveland Cavs ambao ni mabingwa watetezi, 110-106.
“Ilikuwa mechi mbovu na ya ajabu,” alisema LeBron James, ambaye alifunga pointi 23 points baada ya kuwa na pointi 2 tu katika nusu ya kwanza.
Atlanta iliongoza kwa pointi zaidi ya 18 katika robo ya tatu kabla ya  Cleveland hawajapunguza mpaka pointi 2 tu. Hawks wakarejesha uongozi kwa pointi 15 mwanzo wa robo ya nne lakini Cavaliers wakapunguza tena mpaka pointi 2 zikiwa zimesalia sekunde 25.
Kent Bazemore, alifunga pointi 25.
Atlanta ilikuwa imepoteza michezo 11 mfululizo dhidi ya Cleveland, ikiwemo kuondolewa kwa michezo minne katika hatua ya mtoano kwa misimu miwili iliyopita.
Paul Millsap alifunga pointi 21 kwa Atlanta. Dwight Howard, aliwasaidia sana Atlanta kwa kudaka rebound 17.
Kyrie Irving aliiongoza Cleveland akiwa na pointi 29 huku mchezaji Kevin Love akiendelea na msimu mzuri akiwa na pointi 24.

Tuesday, November 8, 2016

Ronaldo na Messi waongoza kwa kulipwa pesa nyingi

Wachezaji Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ndio wachezaji wa mchezo wa soka wanaongoza kwa kulipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa.
Ronaldo analipwa kiasi cha Pauni 365,000 kwa wiki huku akijikusanyia kiasi cha pauni milioni 19,kwa mwaka Nae Lionel Messi analipwa kiasi cha Pauni 365,000 kwa wiki huku nae akipata pauni million 19 kama Ronaldo kwa mwaka.


Wachezaji wengine wanaolipwa pesa nyingi duniani

Gareth Bale (Real Madrid) Pauni 346,000 kwa wiki, Pauni Milioni 18 kwa mwaka
Givanildo Vieira de Sousa maarufu kama Hulk (Shanghai SIPG) Pauni 317,000 kwa wiki Pauni Milioni 16.5 kwa mwaka
Paul Pogba (Manchester United) Pauni 290,000 kwa wiki Pauni Milioni 15 kwa mwaka
Neymar (Barcelona) Pauni 289,000 kwa wiki Pauni Milioni 15 kwa mwaka
Graziano Pelle (Shandong Luneng) Pauni 260,000 kwa wiki Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka
Wayne Rooney (Manchester United) Pauni 260,000 kwa wiki, Pauni Milioni 13.5 kwa mwaka
Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) Pauni 250,000 kwa wiki, Pauni Milioni 13 kwa mwaka
Sergio Aguero (Manchester City) Pauni 240,000 kwa wiki, Pauni Milioni 12.5 kwa mwaka
Yaya Toure (Manchester City) Pauni 240,000 kwa wiki, Pauni Milioni 12.5 kwa mwaka